Psalms 85

Maombi Kwa Ajili Ya Ustawi Wa Taifa

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Wana Wa Kora)


1 aEe Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako.
Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.
Au: Uliwarudisha mateka wa Yakobo.


2 cUlisamehe uovu wa watu wako,
na kufunika dhambi zao zote.

3 dUliweka kando ghadhabu yako yote
na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.


4 eEe Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena,
nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

5 fJe, utatukasirikia milele?
Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?

6 gJe, hutatuhuisha tena,
ili watu wako wakufurahie?

7 hUtuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana,
utupe wokovu wako.


8 iNitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana;
anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake:
lakini nao wasirudie upumbavu.

9 jHakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao,
ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.


10 kUpendo na uaminifu hukutana pamoja,
haki na amani hubusiana.

11 lUaminifu huchipua kutoka nchi,
haki hutazama chini kutoka mbinguni.

12 mNaam, hakika Bwana atatoa kilicho chema,
nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.

13 Haki itatangulia mbele yake
na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.
Copyright information for SwhKC